219 – Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:

“Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimuona bwana mmoja ambaye hakuosha visigino vyake ambapo akasema:

ويلٌ للأعقابِ مِن النارِ

“Ole visigino kutokana na Moto.”[1]

Imekuja katika upokezi mwingine:

“Abu Hurayrah aliona kundi la  watu wanatawadha kutoka ndani ya chombo akasema: “Timizeni vizuri wudhuu´ wenu! Kwani hakika mimi nimemsikia Abul-Qaasim (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akisema:

ويلٌ للأعقابِ مِن النارِ

“Ole visigino kutokana na Moto!”

Ameipokea al-Bukhaariy, Muslim, an-Nasaa´iy pamoja na Ibn Maajah kwa kifupi.

[1] Swahiyh.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Adhwiym bin ´Abdil-Qawiy al-Mundhiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/206)
  • Imechapishwa: 18/01/2024
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy