Hatutoi fatwa za talaka katika vikao hivi

Swali: Bwana mmoja amemwambia mke wake kwamba mafungano kati yao yamekwisha akienda nyumbani kwa mama yake mdogo. Je, maneno haya yanazingatiwa kuwa ni talaka? Nifanye nini na nende wapi?

Jibu: Njoo kesho katika kamati ya kudumu ya kutoa fatwa au mahakamani. Hatutoi fatwa zinazohusiana na mambo ya talaka katika vikao hivi. Ni lazima jambo likaguliwe na kutiwa saini. Kwa mfano mmlitangulia kuachana hapo kabla? Ni lazima kuyaangalia yote hayo kwa ajili ya kuchukua tahadhari.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (42)
  • Imechapishwa: 18/01/2024