Usichaji simu yako kwa moto wa msikiti!

Haijuzu kuchaji simu kutoka katika umeme wa msikiti. Haijuzu kutumia umeme wa msikiti katika mambo binafsi ya mtu. Haijuzu kwa mfano mtu kuunganisha waya ya umeme kutoka msikitini kwenda nyumbani kwake. Msingi kwa mujibu wa wanazuoni ni kwamba mali ya Waqf inatumiwa kwa mujibu wa sharti ya yule aliyejitolea ikiwa ameweka sharti yoyote… Plagi hii ya umeme imewekwa kwa ajili ya huduma za msikiti, kivuta vumbi cha umeme, kipaza sauti na kadhalika. Si sahihi kusema kwamba uwepo wake unawapa ruhusa watu kuzitumia. Kuwafungulia watu mlango huo kutapelekea misikiti kuwa na gharama kubwa. Mtu asiseme kuwa kuchaji simu sio ghali. Badala yake anapaswa kuangalia ile idadi kubwa ya simu za watu.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Ibraahiym Aalush-Shaykh
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (09/70)
  • Imechapishwa: 18/01/2024