Mwenye kuhiji hakujaaliwa kufunga siku kumi katika Dhul-Hijjah

Swali: Mtu mwenye kufanya hajj ya Tamattu´ asiyekuwa na kichinjwa na wala hakufunga siku kumi mpaka ukamalizika mwezi wa Dhul-Hijjah. Ni kipi kinachomlazimu?

Jibu: Ni lazima kwake kuzifunga na wala haziishilii Dhul-Hijjah. Kama hakujaaliwa kufunga siku tatu katika hajj, basi anatakiwa kuzifunga pamoja na siku saba pindi itapomkuia wepesi kufanya hivo.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (16)
  • Imechapishwa: 11/05/2021