Mwanamke wa Kiislamu anatakiwa ajitukuze kwa Hijaab yake

Swali: Ni ipi nasaha yako kwa wanawake juu ya udharura wa kufunika uso na kutoonyesha mapambo. Je, dalili ya kuonyesha uso inajuzu katika baadhi ya nchi?

Jibu: Mwanamke wa Kiislamu ni Muislamu kila mahala. Ni lazima kwake kushikamana na Ahkaam za Kiislamu kila mahala. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mche Allaah popote ulipo.”

Ashikamane na Ahkaam za Kiislamu na miongoni mwazo ni Hijaab. Ajisitiri kwa Hijaab sawa akiwa katika nchi ya Kiislamu au nje ya nchi ya Kiislamu. Yeye ni mwanamke wa Kiislamu. Ajitukuze kwa Dini yake na ashikamane nayo na asiilembekeze kokote pale.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/al_makruf%202-%2011-08-1433.mp3
  • Imechapishwa: 16/06/2015