Swali: Baba yangu na ndugu zangu hawaswali msikitini na ninawanasihi sana lakini hawaitikii. Bali mara nyingi wakati ninaporudi kutoka msikitini ninakuta baba yangu anavuta bangi na anatazama TV. Je, nijiunge na kikao chao baada ya haya? Je, ninapata dhambi kwa kukaa nao au…

Jibu: Ni lazima kwako unawanasihi na uendelee kufanya hivo. Usiwaache. Endelea kuwanasihi na usinyamazie maovu na usikate tamaa juu ya uongofu wao. Kuwa na subira juu ya wao.

Kuhusu kukaa nao, ikiwa unaweza kutoka nyumbani na kueshi mwenyewe itakuwa ni wajibu kwako kutoka nyumbani na usikae nao ilihali wako katika hali hii. Ama ikiwa huwezi kueshi mwenyewe eshi nao na uwe ni mwenye uvumilivu katika kuwanasihi na kuwakataza.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/al_makruf%202-%2011-08-1433.mp3
  • Imechapishwa: 15/06/2015