Swali: Unasemaje kuhusu ambao wanasema kuwa si lazima kwa mwanamke kutambua mambo ya kimfumo na kwamba ni lazima kwake kusoma mambo ya Tawhiyd peke yake?

Jibu: Yanayomlazimu ni kama mwanamme anatakiwa kutambua mambo yanayohusiana na ´Aqiydah, ´ibaadah, tabia, matangamano mazuri na kutekeleza amana. Yanayomlazimu ni kama yale yanayomlazimu mwanamme. Kwa sababu elimu imegawanyika sampuli mbili. Aina ya kwanza ni ile ambayo inamlazimu kila mmoja. Aina nyingine ni ile ambayo ni lazima kwa baadhi ya watu peke yake. Elimu ambayo inamlazimu kila mmoja inawahusu wanamme na wanawake. Elimu yenye kutosheleza ikifanywa na baadhi ya watu basi wengine hawapati dhambi. Hivyo haifai kwa mwanamke kuacha kusoma mambo ya Kishari´ah. Badala yake anatakiwa kusaidiwa juu ya mambo hayo ili awe ni mtambuzi wa mambo yanayohusu dini yake na pia aweze kuwafunza wengine.

  • Mhusika: ´Allaamah Zayd bin Muhammad al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://z-salafi.com/v2/action?s_menu=23&idFatwa=2568
  • Imechapishwa: 27/06/2020