Msimamizi wa familia kuwarekodi familia

Swali: Mimi ni kaka wa ndugu wa kiume na wa kike ambao bado wakingali wadogo. Kwa ajili hiyo mimi natumia kifaa kama simu kinachorekodi kwa ajili ya kuzuia madhara kwa sababu kuzuia madhara kunapatikana kupitia njia hiyo. Unasemaje juu ya kitendo hicho pamoja na kuzingatia ya kwamba hawajui jambo hilo?

Jibu: Naona kuwa kufanya hivo ni katika upelelezi. Haijuzu kwa yeyote kumpeleleza mwengine. Kwa sababu sisi hakuna tunachoangalia isipokuwa ule uinje wa mtu. Iwapo tungelisema tumpeleleze kila mmoja basi tungelichoka sana kwa kufanya hivo na tungelichokesha nyoyo zetu kwa yale tunayosikia na kuyaona. Ikiwa Allaah anasema:

وَلَا تَجَسَّسُوا

“Na wala msipelelezane.”

Baada ya kusema:

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اجْتَنِبُوا كَثِيرًا مِّنَ الظَّنِّ إِنَّ بَعْضَ الظَّنِّ إِثْمٌ ۖ وَلَا تَجَسَّسُوا

“Enyi walioamini!  Jieupusheni na dhana nyingi kwani hakika baadhi ya dhana ni dhambi. Na wala msipelelezane.”[1]

Lakini baba wa nyumba pindi atapoona alama za wazi zinazofahamisha juu ya mawasiliano haya mabaya, katika hali hiyo hapana ubaya akaweka kifaa cha kurekodi pasi na wao kujua. Lakini ni wajibu kwake pale tu atapojua uhalisia wa mambo basi ayachukulie hatua na kuwakemea. Kwa sababu huenda akitaka kuwafuatilia akayasikia mambo mabaya zaidi kuliko yale aliyoyachukia. Hili ni mosi. Kwa mfano akisikia usiku maongezi mabaya basi papohapo asubuhi yake azungumze na yule muhusika na amkaripie. Asisubiri usiku wa pili, usiku wa tatu au usiku wa nne ili kutaka kujua kwa undani wanayofanya. Hili ni kosa. Ni wajibu kwake kufunga njia pale mwanzoni tu. Akifanya kwa namna hii hakuna neno. Ama tuhuma au wasiwasi tu haifai. Lakini akijua kuwa mambo ni ya khatari na kwamba mambo haya yanatokea kwa njia ya kwamba akawa na dhana yenye nguvu kumdhania, basi hakuna neno akategeza kidude hiki ili ahakikishe mambo.

[1] 49:12

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (50) http://binothaimeen.net/content/1139
  • Imechapishwa: 27/06/2020