Swali: Nitangamane vipi na ndugu yangu wa damu ambaye amejiunga na Takfiyriyyuun?

Jibu: Ni lazima kwako umnasihi ndugu yako wa damu, umbainishie dalili na uwaombe wengine wamnasihi, ingawa ni mara chache mno kwa watu hawa kukubali nasaha. Ni kama vile Allaah amewaadhibu juu ya upindaji wao hivyo wakabali hali ya kuwa ni wapotofu mpaka pale watapokutana Naye. Lakin kwa ajili ya kutafuta udhuru kwa Allaah mbainishie dalili ukiwa ni muweza wa kufanya hivo. Vinginevyo mtumie mtu wa kumnasihi. Unaweza pia kumpa kanda ambayo wananasihiwa Takfiyriyyuun. Akiendelea kung´ang´ania basi itakupasa kumwepuka na ujitenge naye mbali umbali uwezao.

  • Mhusika: ´Allaamah Ahmad bin Yahyaa an-Najmiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fath-ur-Rahiym al-Waduud, uk. 252
  • Imechapishwa: 27/06/2020