Mwanamke mwenye hedhi na nifasi anataka kukhitimisha Qur-aan Ramadhaan

Swali: Je, inafaa kwa mwanamke mwenye hedhi na mwenye damu ya uzazi kugusa Qur-aan na kusoma ndani yake khaswa katika mwezi wa Ramadhaan wenye baraka ambao watu wanapupia kukhitimisha Qur-aan?

Jibu: Sijui kizuizi juu ya hilo. Hadiyth isemayo:

“Haigusi Qur-aan isipokuwa aliye msafi.”

Wako wanaosema kuwa kuna Swahabah anayekosekana katika cheni ya wapoezi. Tukikadiria kuwa ni nzuri kwa mkusanyiko wa njia zake inafasiriwa kama alivosema ash-Shawkaaniy katika “Nayl-ul-Awtwaar”:

“Haigusi Qur-aan isipokuwa aliye msafi.”

“Maana yake ni muislamu.”

Kwa maana nyingine haigusi ambaye ni kafiri. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amekataza mtu kusafiri na Qur-aan kwenda katika miji ya maadui.

Kuhusu maneno Yake (Ta´ala):

لَّا يَمَسُّهُ إِلَّا الْمُطَهَّرُونَ

“Hawaigusi isipokuwa waliotwahara.”[1]

Kinachokusudiwa ni Malaika. Hivo ndivo amesema Imaam Maalik katika “al-Muwattwa´”. Akaongezea kwamba Aayah hiyo inafasiriwa na maneno Yake (Ta´ala):

كَلَّا إِنَّهَا تَذْكِرَةٌ فَمَن شَاءَ ذَكَرَهُ فِي صُحُفٍ مُّكَرَّمَةٍ مَّرْفُوعَةٍ مُّطَهَّرَةٍ بِأَيْدِي سَفَرَةٍ كِرَامٍ بَرَرَةٍ

“Sivyo katu! Hakika hizi ni Ukumbusho. Basi atakaye akumbuke. [Zimeandikwa] katika swahifa zilizokirimiwa. Zimetukuzwa na zimetwaharishwa. [Zinazobebwa] mikononi mwa waandishi, watukufu na watiifu.”[2]

Bi maana Malaika. Kama alivosema Mola wetu:

وَمَا تَنَزَّلَتْ بِهِ الشَّيَاطِينُ وَمَا يَنبَغِي لَهُمْ وَمَا يَسْتَطِيعُونَ إِنَّهُمْ عَنِ السَّمْعِ لَمَعْزُولُونَ

”Na wala hawakuteremka nayo [Qur-aan hii] mashaytwaan na wala haipasi kwao na wala hawawezi. Hakika wao bila shaka wametengwa mbali kutokana na kuisikiliza.”[3]

[1] 56:79

[2] 80:11-16

[3] 26:210-212

  • Mhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fadhwaaih wa Naswaaih, uk. 83
  • Imechapishwa: 20/03/2024