Swali: Ni ipi hukumu ya wanawake kutoka hali ya kujipamba na kujitia manukato kwa ajili ya kuswali Tarawiyh hali ya kuamini kwamba wanafanyia kazi maneno Yake Allaah (Ta´ala):

خُذُوا زِينَتَكُمْ عِندَ كُلِّ مَسْجِدٍ

“Chukueni mapambo yenu katika kila swalah.”[1]?

Jibu: Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amewaruhusu wanawake kutoka kwenda kuswali ´Ishaa msikitini kwa sharti watoke hali ya kujisitiri vizuri, kwa maana ya kwamba wamevaa mavazi ambayo hayavutii kuelekezewa macho na pasi na kujitia manukato. Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mwanamke yeyote anayetoka hali ya kujitia manukato ili wanuse harufu yake, basi ni mzinifu.”

[1] 07:31

  • Mhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fadhwaaih wa Naswaaih, uk. 86
  • Imechapishwa: 21/03/2024