Miaka sita ameshindwa kufunga na bado maradhi yanamwandama

Kutoka kwa Muhammad bin Ibraahiym kwenda kwa muheshimiwa X.

السلام عليكم ورحمة الله وبركاته

Tumefikiwa na barua yako unayouliza maswali mawili ambapo moja wapo ni kwamba unadaiwa swawm ya miaka sita kutokana na miezi sita na kwamba mwezi huu unaokuja utakuwa ni wa saba na kwamba huwezi kufunga na kwamba madaktari wamethibitisha kuwa kufunga kunakudhuru. Unauliza juu ya hilo kama unapaswa kulisha chakula au kitu gani?

Jawabu ni kwamba pale itapohakikishwa kuwa swawm inakudhuru na ukaelezwa jambo hilo na daktari mwaminifu basi ni sawa ukachelewesha kulipa deni lako mpaka wakati utakapoweza kulipa pasi na swawm hiyo kuitia khatarini afya yako. Haikudhuru kitu kukusanyikiwa na miezi kadhaa ya swawm, kwa sababu ni mwenye kupewa udhuru juu ya swawm yako – namuomba Allaah akuharakishie kupona kwako. Hakuna kitachokulazimu katika kulisha chakula wala kitu kingine. Ikitokea maradhi hayo yameendelea na madaktari wakathibitisha kuwa maradhi hayo hayatarajiwi kupona, basi utalisha masikini kwa kila siku iliyokupita kiasi cha Mudd[1] ya ngano au nusu ya pishi ya kitu kingine kwa idadi ya siku unazodaiwa.

20/09/1383

[1] al-Fawzaan amesema:

”Kiwango cha Mudd ni gramu 563.” (Mukhtaswar Ahaadiyth-is-Swiyaam, uk. 52-53))

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Ibraahiym Aalush-Shaykh
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (04/201)
  • Imechapishwa: 21/03/2024