Swali: Je, inajuzu kwa mwanamke kufanya ´Umrah pamoja na dada yake na mume wa dada yake na mume wa dada yake akawa ni Mahram wake?

Jibu: Sio Mahram wake. Haijuzu kwake kusafiri pamoja naye hata kama dada yake atashindikizana nao. Sio Mahram wake. Haijuzu kwake kusafiri isipokuwa awe pamoja naye Mahram. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Sio halali kwa mwanamke anayemwamini Allaah na siku ya Mwisho kusafiri isipokuwa awe pamoja naye Mahram.”

Mahram ni yule ambaye ni haramu kwake, sawa kwa nasaba; kama kaka yake, ami yake na mjomba wake, au kwa sababu inayokubalika; kama mfano wa kunyonyesha, baba wa mume wake au mtoto wa mume wake. Kwa sababu mtoto wa mume wake ni Mahram wake pia.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Kitaab Ahaadiyth-il-Fitnah (2) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/ftn–1432-08-16.mp3
  • Imechapishwa: 21/04/2015