Katika hali hii itabidi kumtii kiongozi huyu….

Swali: Vipi kujumuisha baina ya maneno yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Atapokuja mwingine anataka kumpokonya uongozi, kateni shingo la huyo mwingine.”

na baina ya maneno ya wanachuoni kwamba mtu atapowatawala watu kwa nguvu basi ni wajibu kumtii?

Jibu: Huyu ni kiongozi na huyo mwingine ni kiongozi. Pale ambapo watu watakuwa hawana kiongozi na akaja Muislamu na kuwapiga vita wapinzani mpaka akawashinda na wakawa mkusanyiko, katika hali hii itakuwa ni wajibu kumtii.

Ama kuhusu huyu mwingine amekuja hali ya kuwa kuna kiongozi mwingine, anataka kumpokonya uongozi, huyu ndiye anayestahiki kuuawa. Kuhusiana na yule aliyewatawala watu kutokana na nguvu zake, huyu amekuja wakati ambapo watu hawana kiongozi. Akapigana mpaka akashinda na akawa na uongozi, huyu itabidi kumtii ilimradi ni Muislamu.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Kitaab Ahaadiyth-il-Fitnah (3) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/ftn–1432-08-17.mp3
  • Imechapishwa: 21/04/2015