Swali: Ni yapi maoni yako kwa mwenye kusema kuwa kumuombea Du´aa mtawala ni unafiki?

Jibu: Huu ndio unafiki. Maneno yake haya ndio unafiki. Ama kuhusu kumuombea mtawala ni nasaha. Ni katika imani. Hii ni dalili inayoonesha kuwa anamchukia mtawala. Huku ni kwenda kinyume na Sunnah. Sunnah ni kumuombea mtawala maadamu ni Muislamu. Anaombewa uongofu. Hufai kumsifu yale aliyomo, lakini badala yake muombee wema na uongofu. Akitengemaa na Waislamu pia watatengemaa. Wewe ukimuombea kiongozi unakuwa umewaombea Waislamu. Kwa kuwa kiongozi akinyooka rai pia nao wananyooka.

Salaf walikuwa wakiwaombea watawala. Fudhwayl bin ´Iyaadh amesema, hili limepokolewa pia kwa Imaam Ahmad:

“Lau ningelikuwa na uombezi wenye kujibiwa ningelimuombea nao kiongozi.”

Wewe hujaambiwa usifu yale anayoyafanya mpaka useme kuwa ni unafiki. Wewe unamuombea wema na uongofu. Kwa kuwa kufanya hivi kuna manufaa kwa Waislamu. Huku ni kumnasihi mtawala na Waislamu wengine.

Wale wasiompenda mtawala wana uasi na ni madhehebu ya Khawaarij. Wale wasiomuombea Du´aa kiongozi, hili ndio chimbuko la uasi. Huu ndio msingi wa Khawaarij.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Kitaab Ahaadiyth-il-Fitnah (3) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/ftn–1432-08-17.mp3
  • Imechapishwa: 21/04/2015