Swali: Wale wanaokufa katika maandamano wanazingatiwa kuwa ni mashahidi?

Jibu: Hili tunamwachia Allaah (Subhanaahu wa Ta´ala). Sisi hatumhukumu yeyote. Hata mwenye kufa katika uwanja wa Jihaad, hatuhukumu kuwa ni shahidi. Tunatarajia kwake shahaadah. Hatumkatii shahaadah yeyote isipokuwa yule aliyekatiwa na Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ya kwamba ni shahidi. Mtu binafsi hatumkatii shahaadah. Lakini badala yake tunasema yule mwenye kuuawa katika njia ya Allaah ni shahidi, kwa njia ya ujumla. Ama inapokuja kwa mtu binafsi tunasema kuwa tunatarajia shahaadah kwa mtu fulani. Kuhusu kumkatia mtu shahaadah, hili linahitajia dalili. Hii ndio kanuni kwa wanachuoni.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Kitaab Ahaadiyth-il-Fitnah (3) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/ftn–1432-08-17.mp3
  • Imechapishwa: 21/04/2015