Mtoto wa nje ya ndoa anataka mawasiliano na baba yake

Swali: Ni ipi hukumu ya mtu aliyezini katika mji wa magharibi. Baadaye mtoto wake akawa mkubwa. Mtoto huyu anataka kuwa na mawasiliano na baba yake. Mtu huyu ataamili vipi?

Jibu: Huyu sio mtoto wake. Hili halijuzu. Sio mtoto wake. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mtoto ni yule wa kitandani.”

Mtoto ni lazima awe wa ndani ya ndoa. Ama mtoto wa nje ya ndoa, baba yake anatakiwa kupigwa mawe. Mtoto wa uzinzi hanasibishwi kwa yeyote zaidi ya mama yake. Mtoto wa uzinzi ananasibishwa kwa mama yake tu na wala hanasibishwi kwa baba.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Kitaab Ahaadiyth-il-Fitnah (2) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/ftn–1432-08-16.mp3
  • Imechapishwa: 21/04/2015