Mwanamke kupanda kwenye gari na dereva wa kiume – khatari zaidi kuliko kukaa chemba

Swali: Je, mwanamke kupanda gari peke yake na mwanaume wa kando ndani ya mji kunazingatiwa ni kukaa faragha?

Jibu: Naona kuwa huku ni kukaa faragha. Mwanamke kupanda gari na dereva ambaye sio Mahram wake ni faragha ilioharamishwa. Ni kitendo kinachoingia ndani ya maneno ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Mwanaume asikae faragha na mwanamke isipokuwa awe na Mahram.”

“Hakuna mwanaume atakaa faragha na mwanamke isipokuwa watatu wao atakuwa ni shaytwaan.”

Kukaa faragha huku ni khatari zaidi kuliko kukaa faragha kwenye chumba. Hilo ni kwa sababu dereva hucheza na akili ya mwanamke huyu, atampambania maovu, atamlegezea maneno na anaweza kumpeleka anakotaka. Khatari ya huyu ni kubwa zaidi. Kwa hivyo si halali kwa mwanamke anayemwamini Allaah na siku ya Mwisho kupanda na dereva ambaye si Mahram wake hata kama ni ndani ya mji.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa´ ash-Shahriy (74) http://binothaimeen.net/content/1729
  • Imechapishwa: 25/08/2020