Bora waislamu wenyewe ndio wasimamie ujenzi wa misikiti

Swali: Je, inafaa kwa wasiokuwa waislamu kusimamia ujenzi wa misikiti na kuiamirisha pamoja na kuzingatia kwamba kitendo hicho kinapelekea wao kuingia ndani yake na pengine hata kukaa na kuzungumza humo?

Jibu: Haitakikani kuchukulia wepesi jambo hili, kuwaamini makafiri na kuwafanya wakasimamia mambo ya waislamu khaswa jambo la kusimamia zoezi la ujenzi wa misikiti. Zoezi hili linatakiwa kusimamiwa na wafanya kazi waislamu, nao ni wengi. Inatakiwa kujichunga na kujiepusha na jambo kama hili na kuiamirisha, kuijenga na kuiboresha misikiti liachwe kwa wafanya kazi waislamu, nao ni wengi. Kwa hivyo hakuna haja ya kuwaacha na kuwaendea wengine.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.youtube.com/watch?v=1muw6vTdQPk
  • Imechapishwa: 25/08/2020