Swali: Suufiyyah wengi wanatumia hoja kwamba inajuzu kuingiza kaburi msikitini kwa kaburi la Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwamba liko ndani ya msikiti wake. Vipi tutawaraddi?

Jibu: Allaah awakebehi! Utumiaji dalili huu ni wa batili. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hakuzikwa ndani ya msikiti wake. Alizikwa nyumbani kwake ambapo nyumba yake ilikuwa nje ya msikiti. Liliendelea kuwa nje ya msikiti mpaka ulipopanuliwa msikiti wakati wa ´Abdul-Malik bin Marwaan. Gavana wa al-Madiynah alikuwa ni ´Umar bin ´Abdil-´Aziyz (Rahimahu Allaah). Akamuamrisha kuiingiza nyumba ndani ya msikiti. Kwa halikuingia katika zama za Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), Abu Bakr, ´Umar, ´Uthmaan wala wakati wa ´Aliy. Liliingia wakati wa Banuu Umayyah. Hilo halikufanywa kwa fatwa ya wanachuoni. Ilikuwa ni amri ya mtawala na sio kwa fatwa ya wanachuoni.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (43) http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/ighastah%20%20-%2019%20-%201%20-%201437.mp3
  • Imechapishwa: 25/08/2020