Swali: Vitu vya kuchezea vya watoto vimeruhusiwa kwa kuwa mapicha yake yamevuiwa kwa sababu ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa) alicheza na doli ya farasa mwenye mbawa?

Jibu: Kuna wanachuoni ambao wako na maoni haya na kusema kuwa vitu vya kuchezea vya watoto vina neno. Wanatumia hoja kwa kitu cha kuchezea cha ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa). Hata hivyo maoni sahihi ni kwamba haijuzu. Wasiachiwe watoto wakatumia mapicha na masanamu na wakalelewa navyo. Kuna vitu vya kuchezea visivyokuwa mapicha.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (43) http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/ighastah%20%20-%2019%20-%201%20-%201437.mp3
  • Imechapishwa: 25/08/2020