Aina mbili za kutufu kwenye makaburi  

Swali: Nimesoma kwenye kitabu kwamba kuna ainambili za kutufu kwenye makaburi. Aina ya kwanza ikiwa mtu anayefanya hivo anafikiria kuwa ni kitu alichoamrisha Allaah na kwamba ni ´ibaadah kwa ajili ya Allaah ilihali ni mjinga; hii sio shirki kubwa, bali ni maasi na Bid´ah. Aina ya pili akitufu kwa ajili ya kuliadhimisha, kumuomba maiti au kumuomba msaada; hii ni shirki kubwa. Je, upambanuzi huu ni sahihi?

Jibu: Ndio, huu ni upambanuzi sahihi. Haya ndio maneno ya watu wa haki. Kutukufu kwenye makaburi ikiwa anakusudia kumuabudia Allaah ni Bid´ah, kwa sababu Allaah hakuamrisha hili. Ikiwa natukufu kwa kuliabudia lile kaburi ni shirki. Ni jambo liko wazi.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (43) http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/ighastah%20%20-%2019%20-%201%20-%201437.mp3
  • Imechapishwa: 25/08/2020