Mwanamke kuolewa na ambaye wanalingana naye ngazi

Swali: Je, kunawekwa sharti kule wanandoa kuendana na kulingana (الكفاءة) kwa upande wa nasabu zao?

Jibu: Hapana, sio sharti. Walingane kidini:

فَإِنْ عَلِمْتُمُوهُنَّ مُؤْمِنَاتٍ فَلَا تَرْجِعُوهُنَّ إِلَى الْكُفَّارِ ۖ لَا هُنَّ حِلٌّ لَّهُمْ وَلَا هُمْ يَحِلُّونَ لَهُنَّ

“Na mkiwatambua kuwa ni waumini basi msiwarejeshe [Makkah] kwa makafiri – wao si [wake]halali kwao [hao makafiri] na wala wao si [waume]halali kwao.” (60:10)

إِنَّ أَكْرَمَكُمْ عِندَ اللَّـهِ أَتْقَاكُمْ

”Hakika aliye mbora zaidi miongoni mwenu mbele ya Allaah ni yule mwenye kumcha Allaah zaidi kati yenu.” (49:13)

Walingane na kuendana kidini. Muislamu asimuoe mwanamke wa kishirikina, kwa sababu Allaah anasema:

وَلَا تُنكِحُوا الْمُشْرِكِينَ حَتَّىٰ يُؤْمِنُوا

”Na wala msiwaoze wanaume washirikina mpaka waamini.” (02:221)

لَا هُنَّ حِلٌّ لَّهُمْ وَلَا هُمْ يَحِلُّونَ لَهُنَّ

“Wao [wanawake wa kiislamu] si halali kwao [hao makafiri] na wala wao [waume] si halali kwao.” (60:10)

Vivyo hivyo kuna uchambuzi kati ya muungwana na mtumwa.

Swali: Anayesema wa kijani?

Jibu: Hili ni jambo jipya kati ya watu wasiokuwa wasomi. Vinginevyo msingi ni mwarabu na asiyekuwa mwarabu. Huu ndio msingi. Baadhi wanalingana na wengine:

إِنَّ أَكْرَمَكُمْ عِندَ اللَّـهِ أَتْقَاكُمْ

”Hakika aliye mbora zaidi miongoni mwenu mbele ya Allaah ni yule mwenye kumcha Allaah zaidi kati yenu.”

Swali: Baadhi wanajengea hoja maneno ya ´Umar aliyesema:

“Nitawazuia wale wanawake wenye nasabu wasiolewe isipokuwa na wale wanaolingana nao.”?

Jibu: Ikiwa imesihi[1], basi hiyo ni Ijtihaad yake.

[1] adh-Dhahabiy amesema:

”Ndani yake [kwenye cheni yake ya wapokezi yuko al-Haarith bin ´Imraan al-Ja´fariy ambaye anatuhumiwa uwongo na ´Ikrimah amemdhoofisha.” (Talkhiysw ´alaal-Mustadrak (02/02).

Ibn Qudaamah katika ”al-Mughniy” (09/388) amemnukuu Ibn ´Abdil-Barr ambaye amesema:

”Huyu ni mnyonge na hana msingi na wala hakujengewi hoja kwa mtu mfano wake.”

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23212/هل-تشترط-الكفاءة-بين-الزوجين-في-النسب
  • Imechapishwa: 28/11/2023