Mwanamke aombe talaka kwa mume ambaye ni tasa?

Swali: Wanandoa wengi wanaishi pasi na watoto na hilo ni kwa sababu ya tatizo liliopo kwa mume. Je, bora ni mume kutafuta matibabu pamoja na kusubiri na kuatarajia malipo kutoka kwa Allaah au atafute mwanamke mwingine badala?

Jibu: Hapana shaka kwamba kuchelewa kupata mtoto kunawezekana ni kwa sababu mwanaume huyo ni tasa kama ambavyo vilevile kunawezekana kukawa ni kwa tatizo linaloweza kuondoka kwa matibabu. Kwa ajili hiyo tunamnasihi yule ambaye amechelewa kupata mtoto basi ajitibishe kwa madaktari. Kwa sababu kupata watoto wengi ni jambo ambalo linatakiwa na Shari´ah. Kwa hivyo atafute matibabu. Wakisema kuwa ni tasa basi amshukuru Allaah kwa sababu hajui ni kipi chenye manufaa na yeye. Wakisema kuwa hana nguvu za kiume basi atafute vitu vya kumpa nguvu. Kilicho muhimu ni kwamba atafute matibabu kwa madaktari huenda akapata matibabu na hilo halipingani na kumtegemea Allaah. Bali kufanya sababu kunaingia katika utegemezi.

Lakini mimi nimefahamu kitu kingine kupitia swali hili; je, mwanamke huyu asubiri na kutarajia malipo pamoja na mume huyu au aombe kufutwa kwa ndoa? Tunamwambia kwamba atazame manufaa zaidi; manufaa  yakipelekea kubaki pamoja naye katika hali hii basi ni kheri. Akisema kuwa anataka watoto basi amtake radhi na amuombe avunje ndoa au amtaliki.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (50) http://binothaimeen.net/content/1151
  • Imechapishwa: 25/06/2019