1529- Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
”Ardhi itajaa jeuri na dhuluma. Wakati itakapojaa jeuri na dhuluma Allaah atamtuma mtu anayetokamana na mimi; ana jina kama langu. Ataijaza uadilifu kama itavyokuwa imejaa jeuri na dhuluma.”
Ameipokea al-Bazzaar[1], Ibn ´Adiy[2] na Abu Nu´aym[3] kupitia kwa Daawuud bin al-Mihbar…
Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah amesema:
“Hadiyth zinazozungumzia kuhusu kujitokeza kwa al-Mahdiy ni Swahiyh. Amezipokea Abu Daawuud, at-Tirmidhiy, Ahmad na wengineo kupitia kwa Ibn Mas´uud na wengineo.”[4]
Vivyo hivyo ndivo ilivyokuja katika ”al-Muntaqaa min Minhaaj-il-I´tidaal[5]” ya adh-Dhahabiy.
MAimamu hawa wakubwa katika Hadiyth wamesahihisha Hadiyth zinazozungumzia kuhusu kujitokeza kwa al-Mahdiy. Wako wengine wengi waliotangulia na waliokuja nyuma ambao wanaonelea hivo. Kwa sasa naweza kutaja wafuatao:
1 – Abu Daawuud katika ”as-Sunan” kwa vile amenyamazia jambo hilo.
2 – al-´Uqayliy.
3 – Ibn-ul-´Arabiy katika ”´Aaridhat-ul-Ahwadhiy”.
4 – al-Qurtwubiy, kama ilivyotajwa katika ”Akhbaar-ul-Mahdiy” ya as-Suyuutwiy.
5 – at-Twiybiy, kama ilivyotajwa katika ”Mirqaat-ul-Mafaatiyh” ya Shaykh al-Qaariy.
6 – Ibn Qayyim-il-Jawziyyah katika ”al-Manaar al-Muniyf”, kinyume na wale waliomsemea uongo.
7 – Haafidhw Ibn Hajar katika ”Fath-ul-Baariy”.
8 – Abul-Hasan al-Aaburiy katika ”Manaaqib ash-Shaafi´iy”, kama ilivyotajwa katika ”Fath-ul-Baariy”.
9 – Shaykh ´Aliy al-Qaariy katika ”al-Mirqaah”.
10 – ´Allaamah al-Mubaarakfuuriy katika ”Tuhfat-ul-Ahwadhiy”.
Wapo wengine wengi kwelikweli wenye kuonelea hivo.
Baada ya haya si jambo lenye kushangaza kwelikweli kuona Shaykh al-Ghazaaliy amesema katika kitabu chake kipya “al-Mushkilaat”:
“Kutokana na ninavokumbuka tokea kipindi cha wanafunzi wangu ni kwamba hakukupokelewa Hadiyth ya wazi kuhusu al-Mahdiy. Yale yaliyopokelewa waziwazi sio Swahiyh.”[6]
Ni wepi walioyapinga haya? Ni nani aliyekufanya kukumbuka katika kipindi hicho ulipokuwa mwanafunzi? Je, si ni wanafalsafa ambao hawana elimu yoyote katika Hadiyth wala wapokezi? Vinginevyo ni vipi wanachuoni wa Hadiyth wataweza kuthibitisha kitu ambacho kimepingwa na watu hawa? Je, hayo hayakufanyi kurudi kuichunguza nafsi yako juu ya yale uliyohifadhi ukiwa bado ni mwanafunzi na khaswakhaswa katika yale yanayohusiana na Sunnah na Hadiyth na kusahihishwa na kudhoofishwa kwake? Hilo ni bora kwako kuliko kueneza utata juu ya Hadiyth ambazo zimesahihishwa na wanachuoni kwa sababu tu eti ulizisoma ukiwa bado ni mwanafunzi – kutoka kwa watu ambao si wasomi katika maudhui haya!
[1] Uk. 236-237 kwenye ”az-Zawaa-id” ya Ibn Hajar.
[2] al-Kaamil (1/129).
[3] Akhbaar Aswbahaan (2/165).
[4] Minhaaj-us-Sunnah (4/211).
[5] Uk. 534.
[6] Uk. 139.
- Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Silsilat-ul-Ahaadiyth as-Swahiyhah (4/41-42)
- Imechapishwa: 25/06/2019

Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: Silsilat-ul-Ahaadiyth as-Swahiyhah (4/41-42)
Imechapishwa: 25/06/2019
https://firqatunnajia.com/hadiyth-kuhusu-kujitokeza-kwa-al-mahdiy-ni-swahiyh/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)