Mwanamke amepata hedhi wakati wa swalah

Swali: Mwanamke amepata hedhi wakati wa swalah – yaani baada ya kuingia wakati wa swalah. Je, ni lazima kulipa swalah hiyo baada ya kutwaharika?

Jibu: Hapana. Kama ni mwanzoni mwa wakati jibu ni hapana. Hata hivyo ikiwa atatwaharika mwishoni mwa wakati wa swalah ya pili, kwa mfano akatwaharika mwishoni mwa wakati wa ´Ishaa karibu na kuingia al-Fajr, katika hali hii anatakiwa kuswali Maghrib na ´Ishaa. Au kwa mfano anatwaharika mwishoni mwa wakati wa ´Aswr karibu na jua kuzama, katika hali hii anatakiwa kuswali Dhuhr na ´Aswr.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tafsiyr al-Mufasswal (26) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1428-4-6.mp3
  • Imechapishwa: 19/08/2020