Swali: Ikiwa mwanamke aliyeachika talaka tatu ni mjamzito, mwanamme analazimika kumhudumia. Je, matumizi yanaendelea mpaka pale atakapojifungua na kumnyonyesha mtoto?
Jibu: Ndio. Matumizi ya mtoto yanamlazimu baba yake. Mwanamke anayenyonyesha matumizi yake yanamlazimu baba wa mtoto:
وَإِن كُنَّ أُولَاتِ حَمْلٍ فَأَنفِقُوا عَلَيْهِنَّ حَتَّىٰ يَضَعْنَ حَمْلَهُنَّ ۚ فَإِنْ أَرْضَعْنَ لَكُمْ فَآتُوهُنَّ أُجُورَهُنَّ
”Na wakiwa ni wajawazito, basi wapeni matumizi mpaka wazae mimba zao. Na wakikunyonyesheeni, basi wapeni malipo yao.”[1]
[1] 65:06
- Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (40)
- Imechapishwa: 11/05/2023