Anajifungua kitambo kidogo baada ya kufariki kwa mume

Swali: Je, eda ya mwanamke mjamzito inakwisha akijifungua punde tu baada ya mume wake kuaga dunia?

Jibu: Akijifungua kitambo kidogo tu baada kufariki mume wake, imemalizika eda yake:

وَأُولَاتُ الْأَحْمَالِ أَجَلُهُنَّ أَن يَضَعْنَ حَمْلَهُنَّ

”Na wenye mimba muda wao [wa eda] watakapozaa mimba zao.”[1]

Aayah hii ni kwa njia ya kuachia. Akijifungua kitambo kidogo tu baada ya yeye kuaga dunia, basi imemalizika eda yake. Baadhi ya wanazuoni, kama inavyonasibishwa kwa Ibn ´Abbaas (Radhiya Allaahu ´anhumaa), wanaona kuwa anatakiwa kukaa ile eda ndefu zaidi katika eda mbili hizo, lakini haya sio maoni ya jopo la wanazuoni wengi, na isitoshe sio hayaafikiani na udhahiri wa inavosema Aayah.

[1] 65:04

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (40)
  • Imechapishwa: 11/05/2023