Munkar na Nakiyr ni kwa nyumati zote au ummah huu peke yake?

Swali: Maswali ya Munkar na Nakiyr ni maalum juu ya ummah huu?

Jibu: Hili ni jambo linalohitaji kuangaliwa vyema. Maoni ya karibu zaidi ni kwamba ni kwa ajili ya ummah huu tu. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Hakika utapewa mtihani ndani ya makaburi yao… ”

Hili udhahiri wake ni kwamba ni maalum kwa ajili ya ummah huu. Maneno yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

”Hakika nyinyi mtapewa mtihani ndani ya makaburi yenu inayokaribia fitina ya al-Masiyh ad-Dajjaal.”

Udhahiri wake ni kwamba ni maalum kwa ajili ya ummah huu.

Swali: Ummah ambao wanalinganiwa?

Jibu: Wote, ummah wa wanaolinganiwa na walioitikia. Ni yenye kuenea, kwa waumini na makafiri.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/25098/هل-سوال-منكر-ونكير-خاص-بهذه-الامة
  • Imechapishwa: 01/02/2025