Sifa zote njema ni stahiki ya Allaah, Ambaye amefanya dalili ya mapenzi Yake kuwa ni kufuata mwongozo wa Mtume Wake. Amesema (´Azza wa Jall):
قُلْ إِن كُنتُمْ تُحِبُّونَ اللَّـهَ فَاتَّبِعُونِي يُحْبِبْكُمُ اللَّـهُ وَيَغْفِرْ لَكُمْ ذُنُوبَكُمْ ۗ وَاللَّـهُ غَفُورٌ رَّحِيمٌ
“Sema: “Mkiwa mnampenda Allaah, basi nifuateni mimi. Hivyo atakupendeni Allaah na atakusameheni dhambi zenu na Allaah ni Mwingi wa kusamehe, Mwenye kurehemu.”[1]
Swalah na amani ziwe juu ya bwana wetu na kigezo chetu, Muhammad, ambaye imesihi kuwa amesema:
”Swalini kama mlivyoniona ninaswali.”[2]
Na pia juu ya jamaa zake na Maswahabah wake waliompenda, wakamfuata, wakatuwasilishia Hadiyth zake na kuzihifadhi, na pia juu ya wale waliowafuata kwa uongofu wao na wakashikamana na njia yao mpaka siku ya Qiyaamah.
Hiki ni kijitabu cha sita miongoni mwa vile vitabu sita zinazounda kitabu chetu “Tasdiyd-ul-Iswaabah”. Mada ya kijitabu cha kwanza ilikuwa ni kubainisha uzushi na makosa ya wale waandishi waliotaka kutujibu katika kijitabu chao ”al-Iswaabah”. Hata hivyo hawakufanikiwa wala hawakufaulu, kama nilivyobainisha katika kijtabu changu kilichoashiriwa kilikubaliwa na kupokelewa na watu waheshimiwa. Licha ya ufupi wake wameona kuwa ndani yake kuna utafiti wa manufaa ulioungwa mkono na hoja zenye kukinaisha, uadilifu katika kuraddi, usawa katika kukosoa na kujizuia kulipiza kisasi kwa mfano wa dhuluma uliyofanywa. Namuomba Allaah (Tabaarak wa Ta´ala) akikubali kutoka kwetu na atuhifadhie malipo yake mpaka siku ya Marejeo:
يَوْمَ لَا يَنفَعُ مَالٌ وَلَا بَنُونَ إِلَّا مَنْ أَتَى اللَّهَ بِقَلْبٍ سَلِيمٍ
“Siku ambayo hayatofaa mali wa watoto. Isipokuwa yule atakayefika kwa Allaah na moyo uliosalimika.”[3]
Hivyo hapa leo tunawasilisha kwa wasomaji watukufu kijitabu cha pili. Kijitabu hicho ni cha kwanza kati ya vile vijitabu vitano tulivyowaahidini katika vijitabu vilivyotajwa hapo juu, navyo ni:
1 – Swalaat-ut-Taraawiyh
2 – Swalaat-ul-´Iydayn fiyl-Muswalla hiyas-Sunnah
3 – al-Bid´ah
4 – Tahdhiyr-us-Saajid min Ittikhaadh-il-Qubuur Masaajid
5 – at-Tawassul – Anwaa´uh wa Ahkaamuh
Mada ya kijitabu chetu cha leo ni kudurusi swalah ya Taraawiyh kwa njia ya ujumla na kudurusi idadi ya Rak´ah zake kwa njia ya kipekee.
[1] 3:31
[2] al-Bukhaariy (631).
[3] 26:88-89
- Muhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Swalaat-ut-Taraawiyh, uk. 3-4
- Imechapishwa: 02/02/2025

Muhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Swalaat-ut-Taraawiyh, uk. 3-4
Imechapishwa: 02/02/2025
https://firqatunnajia.com/01-namna-hii-ndivo-unathibitisha-mapenzi-yako-kwa-allaah/