Hii ni kwa sababu wale wanaojiita waandishi wamedai katika kijitabu chao, katika ukurasa wa 6, ya kwamba ”idadi ya Rak´ah ishirini zimethibiti kwa sababu makhaliyfah wote, isipokuwa tu Abu Bakr as-Swiddiyq, walihifadhi jambo hilo. Kadhalika wamemnasibishia, katika ukurasa wa 12, ´Umar ”uzushi”. Kuna uwezekano mkubwa kwamba wanakusudia kuwakusanya kwake watu katika swalah ya Tarawiyh, katika ukurasa wa 40 wamemnukuu al-´Izz bin ´Abdis-Salaam juu ya mifano ya Bid´ah zinazopendekezwa, kukiwemo swalah ya Tarawiyh. Pengine Ibn ´Abdis-Salaam (Rahimahu Allaah) anakusudia ni watu kukusanyika kuswali Tarawiyh kwa Rak´ah ishirini[1]. Lakini waandishi wametaja tamko ambalo huenda likafahamika kuwa wao hawoani kuwa kuongeza juu ya yale yaliyopokelewa ni Bid‘ah[2]. Kwa hivyo maana ya ”uzushi” waliyomnasibishia kiongozi wa waumini ´Umar (Radhiya Allaahu ´anh) si kingine isipokuwa ni kule kuwakusanya kwake watu katika swalah ya Tarawiyh. Pasi na kujali nini walichokusudia kwa neno ”uzushi”, kutokana na kwamba hatuoni kuwa ´Umar (Radhiya Allaahu ´anh) hakuzusha kitu ambacho katika swalah hii, si mkusanyiko wala Rak´ah ishirini – kwani yeye alikuwa ni mfano mzuri kabisa wa muumini anayefuata Sunnah za Mtume wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) – na kutokana na kwamba tunaona kuwa haijathibiti kutoka kwa yoyote miongoni mwa makhaliyfah waongofu idadi ya Rak´ah ishirini, basi nikawa sina budi kuwabainishia ukweli huu watu, ili asiwepo yeyote atakayedanganyika na ”uzushi” ambao waandishi wamemsingizia kiongozi wa waumini ijapo wao wanaona kuwa ni kizuri. Haki ya kweli kwa wanazuoni ni kwamba kufuata ni bora kuliko kuzushi hata kama tutakisia kuwa kuna Bid‘ah nzuri! ‘Abdullaah bin Mas‘uud (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:
“Kufanya uwastani katika Sunnah ni bora kuliko kujitahidi katika Bid‘ah.”[3]
[1] Haya yameashiriwa na wanazuoni wengi, akiwemo al-Qastwalaaniy katika “Irshaad-us-Saariy” (4/5).
[2] Uk. 9.
[3] ad-Daarimiy (1/72), al-Bayhaqiy (3/19) na al-Haakim (1/103), ambaye ameisahihisha na ad-Dhahabiy akaafikiana naye. Masimulizi hayo ni Swahiyh.
- Muhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Swalaat-ut-Taraawiyh, uk. 4-7
- Imechapishwa: 02/02/2025

Muhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Swalaat-ut-Taraawiyh, uk. 4-7
Imechapishwa: 02/02/2025
https://firqatunnajia.com/02-umar-hakuzua/