Miongoni mwa mambo yanayothibitisha kuwa waandishi hawa hawako makini katika yale wanayonakili ni kwamba pale walipotumia hoja mgawanyo wa al-‘Izz bin ‘Abdis-Salaam kuhusu Bid‘ah katika mafungu matano walinukuu mifano aliyotoa kwa kila aina isipokuwa tu Bid‘ah inayochukiza. Kwa makusudi kabisa waliondoa kutoka katika maneno ya al-‘Izz mifano aliyotoa kuhusu Bid‘ah hii. al-´Izz amesema:
“Bid‘ah zinazochukiza zina mifano mingi, ikiwa ni pamoja na kupamba misikiti na kupamba misahafu.”
Haitaji akili nyingi ili msomaji aelewe sababu iliyowafanya waandishi hawa kufuta tamko hili kutoka katika maneno ya al-‘Izz bin ‘Abdis-Salaam, khaswa akizingatia kile ambacho mwandishi wa ”al-Iswaabah” alijivunia – ambaye pia ndiye mwenye jukumu kubwa la kitabu hicho – kwani alichapisha kitabu kwa jina lake, huku akiandika kwenye jalada lake ”imamu wa msikiti wa Rawdhwah Dameski”. Msikiti huu ulijengwa kwa juhudi za pamoja za watu wema na wenye heshima, lakini ulipambwa kwa mapambo makubwa mno kwa kudhani kuwa ni ´ibaadah kwa sababu ya kunyamaza waandishi kama hawa na kuficha kwao elimu. ´Abdullaah bin Mas´uud (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:
“Itakuwaje hali yenu mtakapokumbwa na fitina ambayo mzee mkubwa atazeeka nayo, mtoto atakulia nayo na watu wataizingatia kuwa ni Sunnah? Ikiwa sehemu yake itaachwa, bais kutasemwa: ”Sunnah imeachwa.” Wakauliza: “Na lini litatokea hilo?” Akasema: “Watapoondoka wanazuoni wenu, wakawa wengi wasomaji wenu, wanazuoni wenu wa Fiqh wakawa wachache, viongozi wenu wakawa wengi, waaminifu wenu wakawa wachache na watu wakatafuta ulimwengu kwa matendo ya Aakhirah na watu wakasoma kwa lengo lisilokuwa la dini.”[1]
Masimilizi haya, ingawa ni maneno ya Swahabah, lakini yanazingatiwa kuwa na hukumu moja kama maneno ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), kwa sababu kunazungumziwa mambo ya ghaibu ambayo hayawezi kusemwa isipokuwa kwa wahy. Kwa msemo mwingine ni miongoni mwa dalili za unabii wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwani kila tamko ndani yake limethibitika, kama inavyoonekana khaswa katika yale yanayohusiana na Sunnah na Bid‘ah. Utaona kuwa watu wenye pupa zaidi kufuata Sunnah na kupiga vita Bid´ah ndio wanaotuhumiwa na wapinzani kuwa ni wafuasi wa Bid‘ah na waachaji wa Sunnah!
[1] ad-Daarimiy (1/60) kwa cheni mbili ambapo mojawapo ni Swahiyh na nyingine ni nzuri, al-Haakim (4/514) na Ibn ´Abdil-Barr katika “al-Jaamiy´” (1/188).
- Muhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Swalaat-ut-Taraawiyh, uk. 4-5
- Imechapishwa: 02/02/2025

Muhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Swalaat-ut-Taraawiyh, uk. 4-5
Imechapishwa: 02/02/2025
https://firqatunnajia.com/03-unaposoma-kwa-ajili-ya-tumbo/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)