Wako wapi hawa wanaodai kuwatetea Maswahabah kuhusu maneno yake ‘Umar (Radhiya Allaahu ´anh) pale alipotoa amri ya kukarabati msikiti wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa salllam):

“Walindieni watu dhidi ya mvua, lakini jihadharini na kuupaka rangi nyekundu au ya njano.”?

Au maneno yake Ibn ´Abbaas (Radhiya Allaahu ´anhumaa):

“Mtaipamba kama walivyopamba mayahudi na manaswara.”[1]?

Wala haijulikani kuwa kuna Swahabah yeyote aliyewapinga Maswahabah hawa wawili katika jambo hili. Basi watu hawa wawaonyeshe watu kwenda kwao sambamba na Maswahabah katika kukemea kuipamba misikiti na kubainisha kuwa ni miongoni mwa Bid‘ah zinazochukiza, kama alivyosema wazi al-‘Izz bin ‘Abdis-Salaam na wanazuoni wengine wanaotambulika – ikiwa kweli wao ni wakweli katika kuwatetea Maswahabah. Vinginevyo imeshabainika kwa watu kuwa hawakuandika kitabu chao isipokuwa kwa kufuata tu yale ambayo yamezoeleka kwa wengi.

[1] al-Bukhaariy (Mlango wa 62).

  • Muhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swalaat-ul-´Iydayn, uk. 5-6
  • Imechapishwa: 02/02/2025