Swali: Kumeenea kati ya wanawake kitu kinachoitwa “video za kiislamu” ambazo zinaonyesha picha zinazofanya harakati na maonyesho ya Kiislamu. Ni mambo yameingizwa na watu wengi majumbani. Mimi naitaka pia kwa ajili ya watoto lakini mume wangu anakataa kuingiza kifaa hichi nyumbani. Ni ipi hukumu ya hilo?

Jibu: Maamuzi nyumbani yako kwa mume. Kwa sababu nyumba ni nyumba yake na familia ni familia yake. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mwanaume ni mchungi kwa watu wa nyumbani kwake na ataulizwa kwa kile alichokichunga.”

Kama mume wake amekataa kuingiza kifaa hiki, basi ni wajibu kusikiza na kutii. Si halali kwake kukiingiza isipokuwa kwa ridhaa yake. Lakini unachoweza kufanya ni kumkinaisha. Kwa sababu filamu hizi ikiwa ni zenye kuruhusiwa basi hazina neno. Mkinaisha mpaka akinaike kweli na kuridhia. Ama kumlazimisha juu ya hili na kumharibia familia yake mpaka mke akahakikisha amekiingiza ni haramu.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (47) http://binothaimeen.net/content/1081
  • Imechapishwa: 26/03/2019