Wanasema kuwa Anazungumza kwa Utashi na Uwezo Wake. Maneno Yake yamezuka  (حديث) na ndio kitu bora kilichozuka. Hata hivyo wameafikiana kuwa haikuumbwa. Inaweza pia kuitwa (حديث) na (حادث).

Kwa mujibu wa Ahl-us-Sunnah ambao wana kawaida ya kulitumia neno hilo juu ya kiumbe kilichojitenga (kama walivokuwa wakifanya wabishi wakati walipokuwa wakijibizana kuhusu Qur-aan wakati wa fitina ya Imaam Ahamd) haijuzu kusema kuwa Qur-aan ni (حديث). Bali mwenye kusema kuwa Qur-aan (حديث) basi amesema kuwa Qur-aan imeumbwa. Kwa ajili hiyo Imaam Ahmad (Rahimahu Allaah) alimkataza Daawuud kutumia msemo huu. Hivyo wakafikiria wale wanaolitumia kwamba amemkataza kwa sababu hii, jambo ambalo lilikataliwa na maimamu wa Ahl-us-Sunnah. Hata Daawuud mwenyewe haya hayakuwa makusudio yake. Bali yeye na wale wafuasi wake wengine viongozi ni wenye kuafikiana juu ya kwamba maneno ya Allaah hayakuumbwa. Alichokuwa anakusudia ni kwamba yamesimama kivyake, kama walivyokuwa wanaonelea Salaf wengi, akiwemo al-Bukhaariy.

Tofauti kati ya Ahl-us-Sunnah inahusiana na matamshi. Vinginevyo wameafikiana juu ya kwamba sio kiumbe yaliyojitenga na kwamba maneno ya Allaah yamesimama kwenye dhati Yake. Maimamu wa Ahl-us-Sunnah kama mfano wa Ahmad, al-Bukhaariy, Daawuud, Ibn-ul-Mubaarak, Ibn Khuzaymah, ´Uthmaan bin Sa´iyd ad-Daarimiy, Ibn Abiy Shaybah na mfano wao ni wenye kuafikiana juu ya kwamba Allaah anaongea kwa utashi Wake na uwezo Wake. Hata hivyo hakuna yeyote katika wao aliyesema kuwa Qur-aan ni ya kale (milele). Mtu wa kwanza aliyetambulika kusema hivo ni Ibn Kullaab. Imaam Ahmad alikuwa akitahadharisha dhidi ya Kullaabiyyah na akaamrisha al-Haarith bin al-Muhaasibiy asuswe kwa sababu alikuwa ni mmoja katika wao. Hata hivyo imesemekana kuwa al-Haarith alijirudi juu ya maoni yake kuhusu Qur-aan na akasema kuwa Allaah anazungumza kwa sauti. Miongoni mwa walioyasema hayo ni al-Kalaabaadhiy katika ”at-Ta´arruf li Madhhab-it-Taswawwuf”.

  • Mhusika: Shaykh-ul-Islaam Ahmad bin Taymiyyah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (5/532-533)
  • Imechapishwa: 26/03/2019