13. Radd juu ya utata wa kutoacha shirki kwa sababu ya kuwakuta mababu wakifanya hayo

Sababu nyingine pia ni uenezwaji wa shubuha na simulizi ambazo zimewafanya watu wengi kupotea na kuzizingatia kwamba ndio dalili wanazotegemea katika kuyatakasa yale waliyomo. Miongoni mwa shubuha hizi ziko ambazo zilitolewa na washirikina wa nyumati zilizotangulia na ziko zengine ambazo zilitolewa na washirikina wa Ummah huu.

Miongoni mwa shubuha hizo:

Mosi: Ziko shubuha ambazo zinakaribia kuwa ni zenye kushirikiana kati ya mapote ya washirikina katika nyumati mbalimbali tokea hapo kale mpaka hivi sasa. Nayo ni kutumia hoja kwa yale waliyomo mababa na mababu na kwamba wao wamerithi ´Aqiydah hii kutoka kwao. Amesema (Ta´ala):

وَكَذَٰلِكَ مَا أَرْسَلْنَا مِن قَبْلِكَ فِي قَرْيَةٍ مِّن نَّذِيرٍ إِلَّا قَالَ مُتْرَفُوهَا إِنَّا وَجَدْنَا آبَاءَنَا عَلَىٰ أُمَّةٍ وَإِنَّا عَلَىٰ آثَارِهِم مُّقْتَدُونَ

“Hivyo ndivyo hatukutuma kabla yako katika mji mwonyaji yeyote yule isipokuwa wamesema matajiri wake walisema: “Hakika sisi tumewakuta baba zetu juu ya dini na hakika sisi ni wenye kufuata nyao zao.”[1]

Hoja hii hutolewa na kila ambaye ameshindwa kusimamisha dalili juu ya madai yake. Nayo ni hoja batilifu isiyokuwa na uzito wowote katika uwanja wa mjadala. Mababu hawa ambao wanawaiga hawako juu ya uongofu. Wale ambao hali yao ndio hiyo haifai kuwafuata wala kuwaiga. Amesema (Ta´ala):

أَوَلَوْ كَانَ آبَاؤُهُمْ لَا يَعْلَمُونَ شَيْئًا وَلَا يَهْتَدُونَ

“Je, hata kama walikuwa baba zao hawajui chochote na wala hawakuongoka?”[2]

أَوَلَوْ كَانَ آبَاؤُهُمْ لَا يَعْقِلُونَ شَيْئًا وَلَا يَهْتَدُونَ

“Je, hata kama baba zao walikuwa hawaelewi kitu chochote na wala hawakuongoka?”[3]

Kuwaiga mababu kunasemwa vizuri pale ambapo wanapokuwa katika haki. Amesema (Ta´ala) kuhusu Yuusuf (´alayhis-Salaam):

وَاتَّبَعْتُ مِلَّةَ آبَائِي إِبْرَاهِيمَ وَإِسْحَاقَ وَيَعْقُوبَ ۚ مَا كَانَ لَنَا أَن نُّشْرِكَ بِاللَّـهِ مِن شَيْءٍ ۚ ذَٰلِكَ مِن فَضْلِ اللَّـهِ عَلَيْنَا وَعَلَى النَّاسِ وَلَـٰكِنَّ أَكْثَرَ النَّاسِ لَا يَشْكُرُونَ

“Nimefuata mila ya baba zangu; Ibraahiym na Ishaaq na Ya’quub. Haikutupasa kumshirikisha Allaah na kitu chochote. Hiyo ni katika fadhila za Allaah juu yetu na juu ya watu, lakini watu wengi hawashukuru.”[4]

 Amesema (Ta´ala):

وَالَّذِينَ آمَنُوا وَاتَّبَعَتْهُمْ ذُرِّيَّتُهُم بِإِيمَانٍ أَلْحَقْنَا بِهِمْ ذُرِّيَّتَهُمْ

“Wale walioamini na wakafuatwa na kizazi chao kwa imani, Tutawakutanisha na kuwaunganisha na kizazi chao.”[5]

 Shubuha hii imekita kwenye nafsi za washirikina ambapo wanakabili kwayo ulinganizi wa Mitume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Watu wa Nuuh wakati Nuuh (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipowaambia:

فَقَالَ يَا قَوْمِ اعْبُدُوا اللَّـهَ مَا لَكُم مِّنْ إِلَـٰهٍ غَيْرُهُ ۖ أَفَلَا تَتَّقُونَ فَقَالَ الْمَلَأُ الَّذِينَ كَفَرُوا مِن قَوْمِهِ مَا هَـٰذَا إِلَّا بَشَرٌ مِّثْلُكُمْ يُرِيدُ أَن يَتَفَضَّلَ عَلَيْكُمْ وَلَوْ شَاءَ اللَّـهُ لَأَنزَلَ مَلَائِكَةً مَّا سَمِعْنَا بِهَـٰذَا فِي آبَائِنَا الْأَوَّلِينَ

“Akasema: “Enyi watu wangu! Mwabuduni Allaah, kwani hamna mwabudiwa wa haki asiyekuwa Yeye. Je, basi kwa nini hamchi?” Wakasema wakuu waliokufuru miongoni mwa watu wake: “Huyu si chochote isipokuwa ni binaadamu kama nyinyi; anataka ajifadhilishe juu yenu na lau Allaah angelitaka, bila shaka angeliteremsha Malaika. Hatukusikia haya kwa baba zetu wa mwanzo.”[6]

Wameyafanya yale waliyokuwemo mababu zao ni hoja wanayopingana kwayo Mtume wao Nuuh (´alayhis-Salaam).

Watu wa Swaalih walimwambia:

أَتَنْهَانَا أَن نَّعْبُدَ مَا يَعْبُدُ آبَاؤُنَا

“Je, unatukataza kuabudu wale wanaowaabudu baba zetu?”[7]

Watu wa Shu´ayb walimwambia:

أَصَلَاتُكَ تَأْمُرُكَ أَن نَّتْرُكَ مَا يَعْبُدُ آبَاؤُنَا

“Je, swalaah zako zinakuamrisha kuwa sisi tuache wale wanaowaabudu baba zetu?”[8]

Watu wa Ibraahiym pindi alipowaelewesha hoja walimwambia:

إِذْ قَالَ لِأَبِيهِ وَقَوْمِهِ مَا تَعْبُدُونَ قَالُوا نَعْبُدُ أَصْنَامًا فَنَظَلُّ لَهَا عَاكِفِينَ  قَالَ هَلْ يَسْمَعُونَكُمْ إِذْ تَدْعُونَ أَوْ يَنفَعُونَكُمْ أَوْ يَضُرُّونَ قَالُوا بَلْ وَجَدْنَا آبَاءَنَا كَذَٰلِكَ يَفْعَلُونَ

“Alipomwambia baba yake na watu wake: “Mnaabudu nini?” Wakasema: “Tunaabudu masanamu na tutaendelea kuyakalia kwa kuyaabudu.” Akasema: “Je, yanakusikieni mnapoyaomba au yanakunufaisheni au yanakudhuruni?” Wakasema: “Tumewakuta baba zetu wakifanya hivyo.”[9]

Fir´awn alisema kumwambia Muusa:

قَالَ فَمَا بَالُ الْقُرُونِ الْأُولَىٰ

”Akasema: “Basi nini hali ya karne za mwanzo?”[10]

Namna hii ukafiri ni dini moja. Watu wake hawamiliki hoja ambayo kwayo wataikabili haki isipokuwa hoja zisizokuwa na mashiko.

[1] 43:23

[2] 05:104

[3] 02:170

[4] 12:38

[5] 52:21

[6] 23:23-24

[7] 11:62

[8] 11:87

[9] 24:70-74

[10] 20:51

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Bayaan Haqiyqat-it-Tawhiyd, uk. 20-23
  • Imechapishwa: 26/03/2019