Kuna shirki aina mbili:

1- Shirki kubwa inayomtoa mtu katika Uislamu. Ni kama mfano wa kuchinja kwa ajili ya asiyekuwa Allaah, kumuomba asiyekuwa Allaah au kufanya aina yoyote ya ´ibaadah kumtekelezea asiyekuwa Allaah.

2- Shirki ndogo isiyomtoa mtu katika Uislamu. Lakini hata hivyo inapunguza Tawhiyd. Shirki hii inaweza kumpeleka mwenye nayo mpaka mwishowe akatumbukia katika shirki kubwa. Mfano wake ni kama kuapa kwa asiyekuwa Allaah, kujionyesha kwa wingi, kusema “Akitaka Allaah na wewe”, “Lau asingekuwa Allaah na wewe” na mfano wa matamshi kama hayo yanayompitikia mtu kwenye ulimi pasi na kukusudia maana yake.

Shirki imekuwa nyingi katika Ummah huu na jambo lake limeenea kwa sababu ya watu kujiweka mbali na Qur-aan na Sunnah na kuwaiga mababa na mababu juu ya usiokuwa mwongozo. Sababu nyingine ni kuvuka mipaka katika kuwaadhimisha wafu na kuyajengea makaburi yao. Sababu nyingine vilevile ni ujinga juu ya uhakika wa dini ya Uislamu ambayo Allaah katuma kwayo Mtume wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Kiongozi wa waumini ´Umar bin al-Khattwaab (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:

“Kamba ya Uislamu itamegolewa fundo baada ya fundo akikulia katika Uislamu yule asiyejua kipindi kabla ya kuja Uislamu.”

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Bayaan Haqiyqat-it-Tawhiyd, uk. 19-20
  • Imechapishwa: 26/03/2019