Mume anapata dhambi kwa mke wake kutovaa Hijaab?


Swali: Je, mume anapata madhambi ikiwa mke wake havai Hijaab kamilifu na anapuuzia swalah?

Jibu: Mke yuko chini ya usimamizi wa mume wake na yeye ndiye ataulizwa juu yake siku ya Qiyaamah. Allaah (Jalla wa ´Alaa) amesema:

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا قُوا أَنفُسَكُمْ وَأَهْلِيكُمْ نَارًا وَقُودُهَا النَّاسُ وَالْحِجَارَةُ عَلَيْهَا مَلَائِكَةٌ غِلَاظٌ شِدَادٌ لَّا يَعْصُونَ اللَّـهَ مَا أَمَرَهُمْ وَيَفْعَلُونَ مَا يُؤْمَرُونَ

“Enyi mlioamini! Jikingeni nafsi zenu na familia zenu na Moto ambao mafutayake ni watu na mawe; juu yake wako Malaika wakali, shadidi hawamuasi Allaah kwa yale anayowaamrisha na wanafanya yale wanayoamrishwa.” (66:06)

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Nyote ni wachungaji na nyote mtaulizwa juu ya kile mlichokichunga. Kiongozi ni mchungahi na ataulizwa juu ya alichokichunga. Mwanaume ni mchungaji nyumbani kwake na ataulizwa juu ya alichokichunga. Mwanamke ni mchungaji nyumbani kwa mume wake na ataulizwa juu ya alichokichunga. Mtumwa ni mchungaji wa mali ya bwana wake na ataulizwa juu ya alichokichunga. Tanabahini! Nyote ni wachungaji na nyote mtaulizwa juu ya mlichokichunga.”

Mume ataulizwa juu ya mambo yote yanayohusiana na yeye [mke]. Kwa mfano ataulizwa inapokuja katika matumizi, mavazi, makazi na kukaa kwa wema. Hali kadhalika ataulizwa juu yake kwa njia ya kumfunza mambo yanayohusiana na dini yake na kumchunga kwa njia ya kutekeleza yale aliyoamrishwa na Allaah na yale aliyokatazwa na Allaah. Allaah atamuuliza siku ya Qiyaamah juu ya amana hii.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdullaah bin ´Abdir-Rahmaan al-Ghudayyaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Usuwl-is-Sunnah (02)
  • Imechapishwa: 06/09/2020