Mume anachelewesha Fajr kila anapofanya jimaa

Swali: Mume wangu hafanyi jimaa na mimi isipokuwa masaa ya nyuma usiku kwa sababu ya watoto. Kila wakati tunapofanya jimaa haamki kuswali Fajr kwa wakati wake. Nimemnasihi sana na mpaka mara ya mwisho nimemuapia ya kwamba hatoniingilia kwa muda wa wiki. Ni ipi hukumu ya hili? Napata dhambi wakati ambapo tunajamiiana na haamki kuswali Fajr?

Jibu: Jimaa ni haki yake. Huna haki ya kumkatalia. Kuhusiana na kuchelewesha kwake Fajr dhambi na adhabu anapata yeye. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Swalah ngumu kwa wanafiki ni ya ´Ishaa ya Fajr. Lau wangelijua ujira wake, wangelizijia ijapo kama ni kwa kutambaa.”

Mnaweza kufanya jimaa katika mida ya mapema. Si lazima mfanye mida ya nyuma.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdullaah bin ´Abdir-Rahmaan al-Ghudayyaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Usuwl-is-Sunnah (01)
  • Imechapishwa: 06/09/2020