Kazi ya teksi Ulaya

Swali: Je, inajuzu kufanya kazi ya teksi kwa kuzingatia ya kwamba naweza kuwa faragha na mwanamke ndani ya gari au nikabeba wateja walio na pombe au nikawapeleka sehemu ya haramu?

Jibu: Inajuzu kwako kufanya kazi ya teksi. Lakini pamoja na hivyo haijuzu kumbeba mwanamke aliye peke yake ukawa naye faragha na haijuzu kubeba mtu mwenye pombe. Yote haya ni haramu. Haijuzu kwako kufanya hayo.

Ama ukitumia gari yako kwa kubeba vitu ambavyo vimeruhusiwa, ni sawa.

Check Also

Mwanamke anaendeshwa na dereva katika darsa

Swali: Je, inajuzu kwa mwanamke kupanda na dereva ili ahudhurie darsa au ni lazima awe …