Muhammad ´Abduh na al-Ghazaaliy wanakanusha kuwepo kwa Malaika na mashaytwaan

Swali: Umesema kuwa wakanamungu hawa na wanachuoni wa falsafa wanafasiri kuwa Malaika na Mashaytwaan ni mafumbo tu na hakuna viumbe wanaoitwa Malaika wala Mashaytwaan. Vilevile umesema kuwa kuna waislamu leo wanaochukua tafsiri hizi. Je, mwenye kusema hivo anazingatiwa ni muislamu pamoja na kuwa amepinga kuwepo kwa Malaika?

Jibu: Ikiwa ni mwenye kukusudia sio muislamu. Lakini ikiwa ni mwenye kufuata kichwa mchunga au ni mwenye kunukuu anazingatiwa ni mwenye kukosea na anatiwa upotevuni. Lakini hata hivyo hakufurishwi. Anapewa udhuru kwa ujinga wake na kwa kutokukusudia kwake.

Vinginevyo haya yapo katika tafsiyr ya “al-Manaar” kama nilivyokwelezeni. Yamenukuu Muhammad ´Abduh na al-Ghazaaliy. Lakini hata hivyo hatusemi kuwa watu hawa ni makafiri kwa kuwa ni watu wenye kufuata kipofu na wenye kunukuu tu. Sio wao walioanzisha mambo haya kutoka kwao.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Qaa´idah Jaliylah fiyt-Tawassul wal-Wasiylah (29) http://www.alfawzan.af.org.sa/node/2145
  • Imechapishwa: 12/07/2020