Swali: al-Mubdi´, Mwanzilishi ni katika majina ya Allaah (Subhaaah)?

Jibu: Ni Badiy´:

بَدِيعُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ

“Mwanzilishi wa mbingu na ardhi.” (06:101)

Hakukuja tamko al-Mubdi´. Mtu anaweza kulisema kwa njia ya maelezo ya kwamba yeye ndiye Aliyevianzisha na Kuviumba. Kwa njia ya maelezo ni sawa. Ama kufanya katika Majina ya Allaah ni al-Mubdi´ haikuthibiti. Lililothibiti ni Badiy´, mwanzilishi wa mbingu na ardhi na Mwenye kuendesha mbingu na ardhi.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Qaa´idah Jaliylah fiyt-Tawassul wal-Wasiylah (29) http://www.alfawzan.af.org.sa/node/2145
  • Imechapishwa: 12/07/2020