Swali: Kuna wanaosema kuwa Ashaa´irah ni asilimia 95 ya waislamu na kuna wanachuoni wengi na wafikiriaji wengi wa waislamu wanaojinasibisha nao. Ni vipi watakuwa upotofuni?

Jibu: Kinachozingatiwa sio wingi ndugu. Kinachozingatiwa ni nani aliye katika haki hata kama atakuwa ni mtu mmoja peke yake. Kuhusu ambaye hayuko katika haki, hata kama watakuwa ni watu wengi, hawapewi uzito wowote. Amesema (Ta´ala):

وَإِن تُطِعْ أَكْثَرَ مَن فِي الْأَرْضِ يُضِلُّوكَ عَن سَبِيلِ اللَّـهِ

“Ukiwatii wengi walioko katika ardhi, watakupoteza na njia ya Allaah.” (06:116)

Kinachozingatiwa ni yule anayefuata haki na njia sahihi. Wingi hauzingatiwi.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Qaa´idah Jaliylah fiyt-Tawassul wal-Wasiylah (29) http://www.alfawzan.af.org.sa/node/2145
  • Imechapishwa: 12/07/2020