Muadhini acheleweshe adhaana wakati wa kuchelewesha Dhuhr kutokana na jua kali?

Swali: Je, muadhini acheleweshe adhaana wakati wa kuchelewesha Dhuhr?

Jibu: Hakuna kizuizi. Hata kama ataisogeza mbele adhaana asiharakishe kukimu. Hata hivyo itakuwa bora zaidi kuchelewesha adhaana, kama ambavyo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimwamrisha muadhini katika Hadiyth ya Abu Dharr. Kwa sababu watu wakisikia adhaana wanafika wanakuja. Si kila mmoja anajua kuwa imamu atachelewesha Dhuhr. Kwa hivyo akichelewesha adhaana inakuwa ni kuwafanyia upole watu.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23674/هل-يوخر-الاذان-في-حال-الابراد-بالظهر
  • Imechapishwa: 27/03/2024