Miongoni mwa adabu za kisomo ni kumtakasia nia Allaah wakati wa kusoma. Kwa sababu usomaji wa Qur-aan ni katika ´ibaadah tukufu. Hayo tumetangulia kubainisha fadhilah zake. Allaah (Ta´ala) amesema:

فَادْعُوا اللَّـهَ مُخْلِصِينَ لَهُ الدِّينَ

“Basi mwombeni Allaah hali ya kumtakasia Yeye dini.”[1]

فَاعْبُدِ اللَّـهَ مُخْلِصًا لَّهُ الدِّينَ

“Mwabudu Allaah hali ya kumtakasia Yeye dini.”[2]

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Isomeni Qur-aan na tafuteni uso wa Allaah (´Azza wa Jall) kabla ya kuja watu wakaisoma kwa kuiponda; wanatafuta kwayo malipo ya dunia na hawaiharakishi.”

Amepokea Ahmad.

[1] 40:14

[2] 39:02

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majaalis Shahr Ramadhwaan, uk. 93
  • Imechapishwa: 27/03/2024