Kumuitikia muadhini namna hii hakukusihi

Swali: Kusema:

صَدَقْتَ وَبَرِرْتَ

“Umesema kweli na kufanya wema.”

wakati muadhini anaposema kuwa swalah ni bora kuliko usingizi?

Jibu: Hapana. Sawa ni kusema kama anavosema:

الصلاة خير من النوم

“Swalah ni bora kuliko usingizi.”

Kusema hivo hakuna msingi na si sahihi. Aseme kama anavosema muadhini:

الصلاة خير من النوم

“Swalah ni bora kuliko usingizi.”

Wakati wa kukimu aseme kama muadhini:

قد قامت الصلاة

“Swalah imesimama.”

Hivi ndio sawa.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23673/حكم-قول-صدقت-وبررت-في-اجابة-الموذن
  • Imechapishwa: 27/03/2024