03. Hekima na sababu kadhaa za kufanya talaka kuwa mikononi mwa mume

Kwa mujibu wa Hadiyth na maandiko yaliyotangulian kuna dalili ya wazi kwamba talaka inakuwa mkononi mwa mwanaume, ambaye ni mume. Kuna hekima kadhaa zinazofanya talaka kuwa mkononi mwa mwanamme:

1 – Shari´ah yenye hekima imemuwajibishia mume mahari na yeye ndiye akafanywa kuwa mwenye jukumu juu ya watu wa nyumbani kwake; ambaye anapambana kwa ajili yao na kusimamia mambo yao ya wajibu.

2 – Mwanaume ni mtu ambaye ana uwezo wa kudhibiti hisia zake, mvumilivu zaidi na mwenye subira zaidi kuliko mwanameke. Hivyo anakuwa ni mwenye kupupia kuhakikisha zaidi juu ya kudumisha mafunganao ya kindoa.

3 – Mwanaume atabeba matumizi ya kifedha ambayo yatamwandama wakati atakapotoa talaka. Ni mamoja iwe ni katika yale mahari yaliyocheleweshwa, matumizi ya eda, mahari mpya, matumizi ya ndoa mpya kwa mara nyingine na kadhalika.

Kwa sababu hizi ndio maana Allaah akafanya usimamizi kuwa mkononi mwa mwanaume. Amesema (Ta´ala):

الرِّجَالُ قَوَّامُونَ عَلَى النِّسَاءِ بِمَا فَضَّلَ اللَّـهُ بَعْضَهُمْ عَلَىٰ بَعْضٍ وَبِمَا أَنفَقُوا مِنْ أَمْوَالِهِمْ

“Wanaume ni wasimamizi juu ya wanawake kwa kuwa Allaah amefadhilisha baadhi yao kuliko wengine na kwa sababu ya [matumizi] wanayotoa katika mali zao.”[1]

[1] 04:34

  • Mhusika: Shaykh Jamaal bin Furahyaan al-Haarithiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Twalaaq – asbaabuhu wa ´ilaajuh, uk. 18
  • Imechapishwa: 27/03/2024