Mtume ni Mahram wa wanawake wa waumini wa kiume?

Swali: Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa ni Mahram kwa wanawake wa waumini wa kiume?

Jibu: Hapana, hakuwa ni Mahram.

Swali: Kwa sababu utaona baadhi… alikuwa akiegemea jiwe kama mfano wa Umm Sulaym (Radhiya Allaahu ´anhaa) au akiingia nyumbani kwake.

Jibu: Pengine Umm Sulaym (Radhiya Allaahu ´anhaa) alikuwa ni katika mama zake wadogo na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), kama walivosema wanazuoni. Pengine walinyonya pamoja. Vinginevyo hakuna dalili inayofahamisha kuwa yeye (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa ni haramu kwa wanawake wa waumini wa kike.

Swali: Umm Sulaym na Umm Haaniy´?

Jibu: Umm Haaniy ni msichana wa ami yake. Hakuna mahali imetajwa kwamba aliketi naye chemba. Alikuja tu kuuliza.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23256/%D9%87%D9%84-%D9%83%D8%A7%D9%86-%D8%A7%D9%84%D9%86%D8%A8%D9%8A-%EF%B7%BA-%D9%85%D8%AD%D8%B1%D9%85%D8%A7-%D9%84%D9%86%D8%B3%D8%A7%D8%A1-%D8%A7%D9%84%D9%85%D9%88%D9%85%D9%86%D9%8A%D9%86
  • Imechapishwa: 10/12/2023