Swali: Ni ipi hukumu ya kumuweka maiti ndani ya sanduku?

Jibu: Ni jambo halikuwekwa katika Shari´ah. Kilichowekwa katika Shari´ah ni kumuweka ndani ya ardhi. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) walimuweka ndani ya ardhi. Maswahabah walimuweka ndani ya ardhi.

Swali: Ni haramu?

Jibu: Hapana. Angalau kwa uchache… bora ni kuacha kufanya hivo. Inatakiwa kumuweka ndani ya ardhi. Hivo ndivo walivyomfanyia Maswahabah Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Hivo ndivo Maswahabah (Radhiya Allaahu ´anhum) walivokuwa wakifanya.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23252/حكم-وضع-الميت-في-التابوت
  • Imechapishwa: 10/12/2023