03. Hadiyth “Anayekula kitunguu maji au kitunguu saumu basi ajitenge… “

333 – Jaabir (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

مَن أكلَ بصلاً أو ثوماً فلْيَعتزلْنا، أو فليعتزِلْ مساجِدنا، وليَقْعُدْ في بيتِهِ

“Anayekula kitunguu maji au kitunguu saumu basi ajitenge nasi au ajitenge na misikiti yetu na akae nyumbani kwake.”[1]

Ameipokea Muslim, Abu Daawuud, at-Tirmidhiy na an-Nasaa’iy. Kwa Muslim imekuja:

مَن أكل البصلَ والثومَ والكُرّاثَ فلا يقربَنَّ مسجِدنا، فإنَّ الملائكةَ تتأذّى مما يَتأذَى منه بنو آدمَ

“Anayekula kitunguu maji, kitunguu saumu na figili, basi asikurubie msikiti wetu. Kwani Malaika wanakereka na yale yanayowakera wanadamu.”

Imekuja katika upokezi mwingine:

“Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amekataza kula kitunguu maji figili. Ikatokea kuhisi hamu tukala humo mbapo akasema:

مَنْ أكلَ مِنْ هذه الشجرةِ الخَبيثةِ فلا يقربَنَّ مسجدَنا؛ فإنَّ الملائكة تتأذَّى مما يتأذى منه الناس

“Anayekula kutoka katika mti huu mbaya basi asiukurubie msikiti wetu. Kwani Malaika wanakereka na yale yanayowakera watu.”

[1] Swahiyh.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Adhwiym bin ´Abdil-Qawiy al-Mundhiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/254-255)
  • Imechapishwa: 10/12/2023
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy